FANYA YAFUATAYO UKIUMWA NA NYOKA: Kujitibu mwenyewe nyumbani
Автор: WikiElimu
Загружено: 2025-03-14
Просмотров: 748
Описание:
Kuna aina nyingi za nyoka, lakini wapo ambao wana sumu, na hawa ndio wa kuogopwa. Hakuna takwimu za kuaminika kuhusu kiwango cha watu wanaoumwa na nyoka Tanzania, ila inasemekana maeneo ya Northern Tanzania, Arusha na Manyara, yanaongoza kwa kuwa na nyoka wengi. Baadhi ya hawa nyoka ni wafuatao, wengine wana sumu na wengine hawana sumu;
• Black-necked spitting cobras (Naja nigricollis) – anayo sumu – anatema sumu ambayo inaunguza kabisa tishu
• Puff adders (Bitis arietans) – anayo sumu – sumu kali, inaweza kuunguza tishu, kusababisha uvimbe sana na hata kifo
• Common egg-eater (Dasypeltis scabra) – huyu hana sumu - Mara nyingi anakula tu mayai ya ndege kwenye viota
• Rufous-beaked snakes (Ramphiophis rostratus) – Anayo sumu ya kadri – Kwa kawaida huwa si hatari kwa mwanadamu
• Brown house snakes (Lamprophis fuliginosus) – Hana sumu – Hana madhara kwa mwanadamu na mara nyingi utamkuta ndani ya nyumba, anakula panya
• Kenyan sand boa (Eryx colubrinus) – Hana sumu – si hatari – ila huwa anauwa kwa kujizungusha na kujikaza kwa inachotaka kuua
• Black mamba (Dendroaspis polylepis) – Anayo sumu – Ni moja ya nyoka hatari sana duniani – sumu yake inaharibu kabisa mfumo wa fahamu na inaweza kuua kama hutapata matibabu
Mambo ya kufanya ukiwa nyumbani kama umemwa na nyoka
Wataalamu wote wanakubalina ya kwamba, hatua mbili za muhimu zaidi unazotakiwa kufanya ukiwa nyumbani baada ya kuumwa na nyoka ni zifuatazo;
1. Mtambue nyoka aliyekuuma, hata kama haujui jina lake, kama inawezekana kumbuka anavyoonekana
2. Fanya haraka kufika kituo cha afya
Usinyonye sumu kutoka kwenye kidonda au kuchanja kwenye sehemu nyoka aliyouma ili kutoa sumu – njia hii haisaidii. Usiweke barafu kwenye sehemu uliyoumwa na nyoka. Usilale chali, ni muhimu kwamba sehemu uliyoumwa iwe chini kutoka usawa wa moyo wako. Ni vizuri mgonjwa asitumie mguu au mkono ulioumwa na nyoka.
Lakini mambo yote haya, si muhimu kama kuwahi hospitalini kadri inavyowezekana. Usifunge mguu au mkono ulioumwa na nyoka – kufunga kwa muda mrefu kunaweza kuleta madhara zaidi na hata kusababisha ukakatwa mkono au mguu.
Ukifika kwa dakatari
Vituo vya afya vilivyo maeneo hatarishi vina “antivenin kits” zinazosaidia kusawazisha sumu ya nyoka. Daktari atakuuliza ni aina gani ya nyoka aliyekuuma. Matibabu yatategemea uko katika hali gani. Kama nilivyoonesha hapo awali, nyoka wengi hawasababishi madhara, na hata kama wakisababisha wengi hawasababishi kifo.
https://wikielimu.org/
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: