POLISI WATUMIA MABOMU KUTAWANYA WACHIMBAJI
Автор: ITV Tanzania
Загружено: 2026-01-22
Просмотров: 1986
Описание:
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Geita limewatawanya kwa mabomu ya machozi maelfu ya wachimbaji wadogo katika mgodi wa Msasa, wilayani Bukombe, kufuatia mvutano mkubwa kati yao na wamiliki wa mgodi huo.
Wachimbaji hao wanashinikiza kuondolewa kwa tozo ya asilimia 50 ya uzalishaji wa dhahabu na malipo ya shilingi milioni tano kwa kila anayeanza uchimbaji, huku wakitaka kuruhusiwa kuendelea na kazi baada ya uongozi wa mgodi kuzuia shughuli hizo kwa madai kuwa eneo limekuwa hatarishi kutokana na kujaa maji ya mvua.
Hali ya usalama mgodini hapo imekuwa tete huku wachimbaji wakidai kuwa tozo hizo ni kandamizi na zinakwamisha maendeleo yao, wakati wamiliki wakisisitiza usalama wa maisha yao kwanza.
Ripoti kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa mvutano huo umesababisha kusimama kwa shughuli za uzalishaji, huku Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi ili kuzuia uharibifu wa mali na machafuko zaidi wakati suluhu ya kudumu ikitafutwa kati ya pande hizo mbili.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ;
Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania
Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3
Twitter : https://bit.ly/2XG7aii
Instagram : https://bit.ly/34KItmg
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: