MSD inatarajia kuanza kuzalisha ARV nchini kuongeza upatikanaji wa dawa hizo
Автор: UTV Tanzania
Загружено: 2026-02-26
Просмотров: 58
Описание:
Bohara ya Dawa nchini (MSD), kupitia kampuni yake tanzu ya MSD Medipharm inatarajia kuanza uzalishaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi, ARVs, hapa nchini ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Hatua hiyo inakuja kufuatia changamoto ya upatikanaji wa dawa hizo baada ya kupungua kwa misaada kutoka nje ya nchi, hususan Marekani, hali iliyosababisha dawa kuingia kwa kiasi kidogo.
Akizungumza kuhusu mpango huo, Meneja Miradi wa MSD, Elias Katani, amesema kwa sasa dawa za ARV zinanunuliwa kutoka nje ya nchi, lakini taasisi hiyo imeamua kuanza uzalishaji wa ndani ili kuhakikisha upatikanaji unakuwa wa uhakika na endelevu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: