WAKAMATWA WAKIIBA VYUMA DARAJA LA TANZANITE, KAMANDA MULIRO AONYA
Автор: Wasafi Media
Загружено: 2022-04-04
Просмотров: 13274
Описание:
WAKAMATWA WAKIIBA VYUMA DARAJA LA TANZANITE, KAMANDA MULIRO AONYA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa onyo kuwa halitamvumia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha na kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma.
Kamanda wa Polisi Kanda Maluum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro ametoa onyo hilo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwakamata watu wawili waliokuwa wanajaribu kuharibu kwa kukata baadhi ya vyuma vya ngazi moja ya Daraja la Tanzanite lililopo maeneo ya Salender, wilayani Ilala.
Kamanda Muliro amesema, watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi, walikamatwa Aprili 2, 2022 majira ya alfajiri wakiwa wanajaribu kufungua vyuma vilivyopo kwenye nguzo ijulikanayo kama P9 ambayo ipo kwenye daraja hilo. Wote wanahojiwa kwa kina na watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi.
WATCH WASAFI TV📺
AZAM - 411 | DSTV - 296 | ZUKU - 028 | STAR TIMES - 444 & 333 | COCONUT TV - 20 | DODOMA CABLE - 113
LISTEN WASAFI FM 📻
88.9 DAR/ZNZ/PWANI 📻 | 104.1 DODOMA 📻 | 94.5 ARUSHA 📻 | 97.3 MBEYA 📻 | 94.9 MWANZA 📻 | SHINYANGA 106.3 📻 | KIGOMA 101.7 📻
Follow Us On:
INSTAGRAM: / wasafitv || / wasafifm
TWITTER: / wasafitv || / wasafifm
FACEBOOK: / wasafitv
𝑪𝒐𝒑𝒚𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕 ©2021 𝑾𝒂𝒔𝒂𝒇𝒊 𝑴𝒆𝒅𝒊𝒂. 𝑨𝒍𝒍 𝒓𝒊𝒈𝒉𝒕𝒔 𝒓𝒆𝒔𝒆𝒓𝒗𝒆𝒅.
#wasafi #wasafitv #wasafifm
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: