Iddi Pazzy: Ali Kiba, wewe ni mwanamichezo, tunga wimbo wa kuwahamasisha wenzio!...
Автор: MUZIKI NA WANAMUZIKI
Загружено: 2020-09-04
Просмотров: 1627
Описание:
Hapa "GUGO WA MUZIKI" Adam Zuberi katika MUZIKI NA WANAMUZIKI, anaongea na Golikipa wa zamani wa timu ya Taifa TAIFA STARS Iddi Pazzy. Iddi Pazzy anatueleza ilikuwaje wimbo huo uliojulikana kwa jina la 'TAIFA STARS HOYE!' uliotungwa na Mwanamuziki mkongwe na mahiri aliyekuwa kiongozi wa Bendi ya Orchestra Safari Sound OSS na pia aliyejulikana sana kwa umahiri wake wa kucharaza Gitaa lake la nyuzi 12 lililoitwa KOMBORA. Iddi Pazzy pia amemshauri Ali Kiba kutunga wimbo wa kuhamasisha michezo kama walivyokwishafanya wanamuziki wakongwe kama Mbaraka Mwinshehe Mwaruka na Freddy Ndala Kasheba, hasa kwa kuzingatia kuwa Ali Kiba mwenyewe pia ni mwanamichezo.
Ni matumaini ya channel hii ya MUZIKI NA WANAMUZIKI kuwa utafurahia mahojiano haya na Mkongwe huyu wa Soka wa timu ya Taifa ya Tanzania Iddi Pazzy au FATHER kama alivyopachikwa jina hilo na mashabiki wa Soka wa wakati huo. Pia pamoja na kuelimika vilivyo katika video hii, ni matarajio yetu kuwa utaburudika vilivyo na wimbo huo wa TAIFA STARS HOYE! ulioungurumishwa na kikosi cha Safari Sound chini ya kiongozi wake Freddy Ndala Kasheba.
Kama utakuwa na swali, maoni, ushauri au hata ukosoaji, jisikie huru kutoa maoni yako ilimradi tu yasiwe na matusi. Nasi tutajibu kadri tukavyoweza pale inapohitajika kujibu.
Ili usipitwe na habari yoyote ile itakayotundikwa kwenye channel hii, tafadhali click link ifuatayo ili uweze kuwa wa kwanza kujulishwa kuhusu habari mpya
MUZIKI NA WANAMUZIKI:
/ @muzikinawanamuziki
Fresh Jumbe YouTube
/ freshjmw
Adam Zuberi Facebook
https://www.facebook.com/profile.php?...
Fresh Jumbe Facebook
/ akida.mtwana
Website
https://freshjumbe.com/
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: