BOLT YATOA TAMKO ZITO KWA MADEREVA WANAOPEANA AKAUNTI ZA BOLT KUSAFIRISHIA ABIRIA
Автор: Mtanzania Digital
Загружено: 2025-03-05
Просмотров: 1692
Описание:
Bolt, jukwaa linaloongoza katika huduma za usafiri wa mtandaoni, linathibitisha rasmi kwamba punguzo linalotolewa kwa abiria linagharamiwa kikamilifu na Bolt.
Taarifa hii inakuja wakati ambapo kuna dhana potofu kuhusu punguzo la safari zinazotolewa kwa abiria. Wengi wanadhani kuwa punguzo hizi zinaathiri mapato ya madereva, lakini kampuni inafafanua kuwa hali ni kinyume na mawazo hayo.
“Abiria anapopata punguzo kwenye nauli, Bolt hulipa dereva mara moja kwa kiasi kilichopunguzwa. Malipo haya huonyeshwa papo hapo kwenye mapato ya dereva, kuhakikisha kuwa hakuna hasara yoyote ya kifedha inayopatikana. Tumebuni mfumo huu kwa uwazi ili madereva waweze kufuatilia mapato yao kwa urahisi kupitia programu ya Bolt kwa madereva,” amesema Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Kenya na Tanzania.
"Licha ya hatua hizi, bado kuna madai yanayoendelea kuwa punguzo la Bolt linapunguza mapato ya madereva. Hata hivyo, ukweli ni kwamba madereva hupokea nauli kamili kabla ya Bolt kukata kiwango chake cha kawaida cha kamisheni. Kwa bahati mbaya, upotoshaji huu umeleta mvutano usio wa lazima kati ya madereva na abiria, na mara nyingine kusababisha migogoro wakati wa safari," ameongeza Kanyankole.
🛑 Sasa Tumekufikia
🛑Tutahakikisha kila siku unapata habari za ukweli na uhakika.
🛑Ahadi yetu kwenu kuwa watumishi wa kihabari kwenu
🛑 Kama una tukio la Kihabari tupigie +225 767 580 313
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: