HOTUBA YA DAS SANGA KWA MADIWANI WA TUNDURU.
Автор: tunduru_dc
Загружено: 2026-02-12
Просмотров: 78
Описание:
Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru, Ndg.Milongo Sanga akitoa Hotuba wakati akifunga mafunzo ya siku mbili (2) ya kuwajengea uwezo yaliyolenga kuimarisha utendaji kazi, usimamizi wa miradi ya maendeleo na utoaji bora wa huduma kwa wananchi.
Kupitia mafunzo hayo, Waheshimiwa Madiwani wanapata fursa ya kuimarisha uelewa wao katika maeneo mbalimbali ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo, matumizi sahihi ya rasilimali za umma, maadili ya uongozi, pamoja na namna bora ya kushirikiana na watendaji wa Halmashauri ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Pia, Mafunzo hayo yamewapa Madiwani uelewa mpana kuhusu majukumu yao ya kisheria na kiutendaji, ili kuongeza ufanisi katika kusimamia maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika maeneo yao ya uwakilishi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: