ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

ROZARI YA MATESO SABA YA MAMA BIKIRA MARIA | SEVEN SORROWS OF VIRGIN MARY

Автор: lucid tv

Загружено: 2020-11-13

Просмотров: 345322

Описание: ROSARI YA MACHUNGU SABA YA BIKIRA MARIA

Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina

Sala ya kwanza

Ee Mungu wangu, nakutolea Rosali hii ya machungu saba ya Bikira Maria kwa ajili ya utukufu wako na kwa heshima ya mama yako Mtakatifu sana. Nitawaza na kushikania naye katika haya aliyopata. Nawe Maria Mama yetu nakuomba, kwa heshima ya machozi uliyomwaga wakati ulipopatwa na machungu haya, utujalie kutubu dhambi zetu. Amina.

Salamu Maria X 3

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.

UCHUNGU WA KWANZA (LK 2:25-35)
Katika uchungu wa kwanza tunakumbuka wakati mzee mtakatifu Simeoni alipomtabiria Maria kwamba upanga wa uchungu utaufuma moyo wake, akimaanisha mateso na kufa kwake Yesu Kristo mwanae.
Tuombe neema ya kuvumilia mateso.

Baba Yetu x 1
Salamu Maria x 7
Atukuzwe Baba,

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.

UCHUNGU WA PILI (MT 2:12-18)
Katika uchungu wa pili tunakumbuka wakati Maria alipolazimika kukimbilia Misri kwasababu Herode katili alitaka kumuua mtoto Yesu.
Tuombe neema ili miili yetu iwe kimbilio lake Yesu.

Baba Yetu x1
Salamu Maria x7

Atukuzwe Baba,

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.

UCHUNGU WA TATU (LK 2:41-51)
Katika uchungu wa tatu tunakumbuka wakati Maria alipompotezs mwanae mpendwa na kwa siku tatu akamtafuta kwa uchungu mpevu na machozi.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu.

Baba Yetu x 1
Salamu Maria x7

Atukuzwe Baba

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.

UCHUNGU WA NNE (LK 23:26-31)
Katika uchungu wa nne tunakumbuka wakati Maria alipokutana na mwanae wa pekee akiwa amebeba msalaba akielekea mlima Kalvari ambako alikua akienda kusulubiwa kwa ajili ya wokovu wetu.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote.

Baba Yetu x1.

Salamu Maria, x7

Atukuzwe Baba,

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.

UCHUNGU WA TANO (YOHN 19:25-27)
Katika uchungu wa tano tunakumbuka wakati Maria alipomwona mwanae Yesu ametundikwa juu ya msalaba na damu nyingi ikimwagika kutoka sehemu zote wa mwili wake.
Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Maria.

Baba Yetu x1

Salamu Maria, x7

Atukuzwe Baba,

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.

UCHUNGU WA SITA (YHN 19:38-40)
Katika uchungu wa sita tunakumbuka wakati Maria alipomwona askari akimchoma mwanae ubavuni kwa mkuki na wakati mwili wa Yesu, baada ya kusgushwa msalabani, ulipolazwa mikononi mwake.
Tuombe neema ya kutotenda dhambi.

Baba Yetu x1
Salamu Maria, x7

Atukuzwe Baba,

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.

UCHUNGU WA SABA (THN 19:40-41)
Katika uchungu wa saba tunakumbuka wakati Maria alipoona mwili wa mwanae wa pekee Yesu ukizikwa kaburini akitengana na mwanae ambaye kweli alimpenda mno.
Tuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria.

Baba Yetu x1.

Salamu Maria, x7

Atukuzwe Baba,

Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
TUOMBE:
Ee Bwana Mungu wetu, kwa njia ya mateso na kifo cha Mwokozi wetu Yesu Kristu na kwa masumbuko yaliyompata mama yake Bikira Maria, ulileta wokovu kwetu sisi wakosefu. Twakuomba utujalie huu wokovu, tupate kuacha njia za dhambi na kupata yote mema aliyotuahidia Yesu Kristo yeye anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu sasa na milele. Amina.

KUMBUKA
Kumbuka , Ee Bikira Maria, mwenye rehema, haijasikilika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, akiomba msaada wako, akitaka umuombee. Nami kwa matumaini hayo ninakukimbilia ee Mama Bikira mkuu wa Mabikira, ninakuja kwako, ninasimama mbele yako nikilalamika mimi mkosefu, Ee Mama wa Neno la Mungu, usikatae Maneno yangu, bali uyasikilize kwa wema na unitimizie. Amina.

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
ROZARI YA MATESO SABA YA MAMA BIKIRA MARIA | SEVEN SORROWS OF VIRGIN MARY

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

ROZARI YA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU

ROZARI YA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU

⚡️ Военные оставили крупный город || Президента призвали бежать

⚡️ Военные оставили крупный город || Президента призвали бежать

Rozari Matendo ya Mwanga. Rozari ya Alhamisi.

Rozari Matendo ya Mwanga. Rozari ya Alhamisi.

ROZARI YA MACHUNGU SABA YA BIKIRA MARIA | THE SEVEN SORROWS OF MARY | SEVEN DOLORS OF MARY

ROZARI YA MACHUNGU SABA YA BIKIRA MARIA | THE SEVEN SORROWS OF MARY | SEVEN DOLORS OF MARY

SALA YA ASUBUHI

SALA YA ASUBUHI

Псалом 26, 50, 90. Сильная защитная молитва от всех злых людей, врагов, опасностей и грехов. 40 раз

Псалом 26, 50, 90. Сильная защитная молитва от всех злых людей, врагов, опасностей и грехов. 40 раз

NYIMBO ZA MAMA BIKIRA MARIA | BIKIRA MARIA SONGS MIX

NYIMBO ZA MAMA BIKIRA MARIA | BIKIRA MARIA SONGS MIX

Rozari Takatifu Matendo Ya Furaha - Sali Sala Hii Siku ya Jumatatu na Jumamosi.

Rozari Takatifu Matendo Ya Furaha - Sali Sala Hii Siku ya Jumatatu na Jumamosi.

12 января МАТРОНУШКЕ ВКЛЮЧИ Самая Сильная Молитва Матроне Московской о помощи праздник Православие

12 января МАТРОНУШКЕ ВКЛЮЧИ Самая Сильная Молитва Матроне Московской о помощи праздник Православие

ROZARI YA MOYO MTAKATIFU WA YESU | CHAPLET OF SACRED HEART OF JESUS

ROZARI YA MOYO MTAKATIFU WA YESU | CHAPLET OF SACRED HEART OF JESUS

𝐑𝐨𝐳𝐚𝐫𝐢 𝐓𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢𝐟𝐮( 𝐌𝐚𝐭𝐞𝐧𝐝𝐨 𝐲𝐚 𝐅𝐮𝐫𝐚𝐡𝐚-𝐉𝐮𝐦𝐚𝐭𝐚𝐭𝐮 𝐧𝐚 𝐉𝐮𝐦𝐚𝐦𝐨𝐬𝐢)

𝐑𝐨𝐳𝐚𝐫𝐢 𝐓𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢𝐟𝐮( 𝐌𝐚𝐭𝐞𝐧𝐝𝐨 𝐲𝐚 𝐅𝐮𝐫𝐚𝐡𝐚-𝐉𝐮𝐦𝐚𝐭𝐚𝐭𝐮 𝐧𝐚 𝐉𝐮𝐦𝐚𝐦𝐨𝐬𝐢)

Divine Mercy Chaplet (Swahili)

Divine Mercy Chaplet (Swahili)

ROZARI YA DAMU AZIZI YA YESU KRISTO (1) // Valeriana Simon

ROZARI YA DAMU AZIZI YA YESU KRISTO (1) // Valeriana Simon

FUATISHA MAOMBI HAYA KILA SIKU ASUBUHI NA MAPEMA

FUATISHA MAOMBI HAYA KILA SIKU ASUBUHI NA MAPEMA

#Mix: Nyimbo Zote za Mama Bikira Maria | Mwezi wa Rozari - 3 Hours Non Stop

#Mix: Nyimbo Zote za Mama Bikira Maria | Mwezi wa Rozari - 3 Hours Non Stop

ЗА УСОПШИХ 12 января они сильно просят и ЖДУТ! Станут на защиту рода! Молитва За упокой Панихида

ЗА УСОПШИХ 12 января они сильно просят и ЖДУТ! Станут на защиту рода! Молитва За упокой Панихида

MAOMBI YA UKOMBOZI KWA DAMU YA YESU | Deliverance Prayers - Innocent Morris

MAOMBI YA UKOMBOZI KWA DAMU YA YESU | Deliverance Prayers - Innocent Morris

ROZARI TAKATIFU MATENDO YA UCHUNGU

ROZARI TAKATIFU MATENDO YA UCHUNGU

NYIMBO ZA EKARISTI TAKATIFU  (KOMUNIO) ZINAZOIMBWA ZAIDI.WAIMBAJI CHANG'OMBE CATHOLIC SINGERS DSM TZ

NYIMBO ZA EKARISTI TAKATIFU (KOMUNIO) ZINAZOIMBWA ZAIDI.WAIMBAJI CHANG'OMBE CATHOLIC SINGERS DSM TZ

ROZARI TAKATIFU MATENDO YA FURAHA  (Jumatatu na Jumamosi)

ROZARI TAKATIFU MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]