SARAH SULEIMAN ATANGAZA RASMI AZMA YA KUWANIA KITI CHA UWAKILISHI WA WADI YA BULA PESA 2027
Автор: 𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕
Загружено: 2026-02-17
Просмотров: 272
Описание:
Huku kukiwa na takriban mwaka mmoja kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, kinyang’anyiro cha wadhifa wa uwakilishi katika Wadi ya Bula Pesa kinaendelea kupamba moto, kikivutia wawaniaji mbalimbali. Wa hivi punde ni Sarah Suleiman, ambaye ametangaza rasmi azma yake ya kuwania kiti hicho.
Akizungumza na meza ya runinga ya Waso TV baada ya kutangamana na watengenezaji wa bidhaa za vyuma katika eneo la Tum Tum, Sarah amesema endapo atachaguliwa, dhamira yake kuu ni kuwahudumia wakazi wa Bula Pesa kwa usawa, bila ubaguzi wowote.
Aidha, ametoa wito kwa Rais William Ruto pamoja na Gavana Abdi Ibrahim Hassan kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha sekta ya utengezaji wa vyuma katika soko hilo, hatua ambayo amesema itaongeza ajira, kuinua kipato cha wakazi na kukuza uchumi wa eneo hilo.
Katika hotuba yake, Sarah pia amesisitiza umuhimu wa kuwaelekeza vijana katika vituo vya kurekebisha tabia (rehabilitation), akibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kupambana na changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana.
Kwa upande wake, Abdullahi Mohamed almaarufu Abshemo amesema kuwa wanamuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kuwania urais kwa muhula wa pili, huku akithibitisha pia kumuunga mkono Sarah Suleiman katika safari yake ya kisiasa.
Naye Michael Gikundi, ambaye ni mhunzi kwa kimombo black smith katika soko hilo, ametoa wito kwa serikali ya kitaifa na ya kaunti kuwasaidia kwa kuwapatia mashine za kisasa, akisema hatua hiyo itaongeza ubora wa bidhaa zao na kupanua masoko.
Ripoti hii inaashiria mwanzo wa safari ya kisiasa ya Sarah Suleiman, huku wakazi wa Bula Pesa wakisubiri kuona mwelekeo wa ushindani kuelekea uchaguzi wa 2027.
Join this channel to get access to perks:
/ @wasotv
WASO TV - Informing and Entertaining
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: