KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYERS 02/01/2026
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2026-01-02
Просмотров: 516
Описание:
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - FRIDAY PRAYERS 02/01/2026
UJUMBE WA LEO: "NGUVU YA KUNGOJA"
UJUMBE WA LEO:"NGUVU YA KUNGOJA"
Isaya 40 : 31
Kutoka 14 : 13 - 14
Mwanzo 37 : 2, 5
Mwanzo 41 : 46
1 Samwel 1 : 10 - 11, 17, 20
Warumi 4 : 18 - 19
Waebrania 10 : 39
Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Kutoka 14 : 13 - 14
13 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
14 Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Mwanzo 37 : 2, 5
2 Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya.
5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia;
Mwanzo 41 : 46
46 Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi yote ya Misri.
1 Samwel 1 : 10 - 11, 17, 20
10 Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana.
11 Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.
17 Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana.
Warumi 4 : 18 - 19
18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
Waebrania 10 : 39
39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.
1. Unahitaji Neema, Msaada na Nguvu ya KUNGOJA ili uweze kufika pale Mungu anataka 2026
2. Huwezi Kupigana Mwenyewe Vita unayokutana nayo katika maisha yako jifunze Kumtengenezea Bwana Mazingira ili yeye akupiganiye Mwenyewe
ANGENDA ZA MAOMBI
1. TOBA (Hasa kwa Kupoteza Imani wakati wa Kumngoja Bwana na Ahadi zake)
2. Mshukuru Mungu kwa Kuuona 2026
3. Omba Mungu akuoneshe na Kukufundisha Njia yake 2026. Zaburi 32:8
Zaburi 32 : 8
8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
4. Omba Neema, Msaada na Nguvu ya KUNGOJA
Mhubiri: Mwl. Eng Goodluck Mushi
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: