USIAMINI KILA UNACHOKIONA: Kuwa Makini na Maudhui ya AI | LENZI | Michael Kamukulu
Автор: LENZI | Michael Kamukulu
Загружено: 2024-03-02
Просмотров: 2034
Описание:
Usiamini kila unachokiona au kusikia kwenye mitandao. Baadhi ya Maudhui yamezalishwa au kutengenezwa kwa kutumia Artificial Inteligence (AI); kwa Kiswahili tunaita Akili Bandia au Akili Mnemba. Kuwa Makini na Maudhui ya AI.
Tumeona video inayomwonesha Rais wa Kenya Mh. William Ruto akitoa hotuba kwa lugha ya KIFARANSA wakati uhalisia ni kwamba Mh. Ruto haoigei kifaransa. Hotuba yake ilitafsiriwa kwa kutumia teknolojia ya AI na kumuonesha akiongea lugha asiyoijua kwa ufasaha mkubwa.
Kutokana na hatari zinazoambatana na aina hii ya teknolojia, kuna haja na umuhimu wa kuwa makini na kuchukua tahadhari stahiki ikiwemo:
1. Kujielimisha kuhusu AI (Akili Bandia), matumizi yake, faida, hasara na fursa zake;
2. Kujifunza kuchunguza na kuchukua tahadhari kabla ya kuyaamini maudhui yoyote kwenye mitandao;
3. Kutunza taarifa binafsi kwa usalama tuwapo kwenye mitandao.
source: @trtafrika @dayoyusuf3556
Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI @lenzi.michaelkamukulu
Chapters
00:00 Ruto Akiongea kwa Kifaransa (na AI)
00:39 Hatari za matumizi ya AI
01:29 1. Jielimishe kuhusu AI
02:02 2. Fahamu Chanzo cha Maudhui
02:43 3. Tunza taarifa zako kwa usalama mtandaoni
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: