JEMEDARI, POPPAT WANG’AA MIRAMBO ATUPIA KAHAMA
Автор: Daily News Digital
Загружено: 2026-02-27
Просмотров: 165
Описание:
KAHAMA, Shinyanga: MKUTANO Mkuu wa 20 wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) umeendelea kuvuta hisia za wadau wa soka huku vigogo wa mchezo huo wakionekana kung’ara ndani ya Manispaa ya Kahama.
Aliyekuwa mchezaji wa zamani na kiongozi wa mpira ngazi ya vilabu na shirikisho, Jemedari Kazumari, alikuwa miongoni mwa nyota waliopendeza kwenye bonanza maalum lililowakutanisha Kahama Veteran na Wadau wa TFF. Uzoefu wake ulionekana wazi uwanjani huku akiongoza safu kwa utulivu na mbinu.
Kwa upande wa viongozi, Makamu wa Rais wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Poppat', naye ameonesha uimara wake hauishii tu kwenye uongozi bali hali kulisukuma gozi la ng’ombe uwanjani huku akiwaacha mashabiki wengi vinywa wazi.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Oscar Mirambo, alitupia kambani katika mchezo huo wa kirafiki, akiongeza ladha ya ushindani na kuthibitisha kuwa viongozi nao wana kipaji cha kucheza.
Katika pambano hilo lililokuwa na burudani ya aina yake, Kahama Veteran waliibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Wadau wa TFF, huku mashabiki wakishuhudia soka la kuvutia na la kirafiki.
Matukio hayo ni sehemu ya shamrashamra zinazoendelea kuelekea Mkutano Mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Februari 28 ndani ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, ambapo ajenda mbalimbali za maendeleo ya mpira wa miguu nchini zinatarajiwa kujadiliwa.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: / spotileo-176. .
HabariLeo: / habarileo
DailyNews: / dailynewstz
INSTAGRAM;
HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig...
SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: