ULEGA USO KWA USO NA VIGOGO WA CHINA
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-03-26
Просмотров: 892
Описание:
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amekutana na viongozi wakuu wa kampuni kutoka China zinazosimamia miradi ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT), madaraja pamoja na barabara hapa nchini kwa lengo la kutafuta suluhisho la miradi inayosuasua kukamilika.
Mazungumzo ya waziri huyo na vigogo hao yamefanyika leo Jumatano, Machi 26, 2025 katika Ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) jijini Dar es Salaam ambapo pande zote mbili zimefikia makubaliano kuhusu maendeleo ya miradi hiyo.
Akizungumza baada ya kikao hicho, Waziri Ulega amesema mkutano huo ni mwendelezo wa hatua alizochukua baada ya ziara yake ya Machi 4, 2025, ambapo alikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya BRT4 ambapo makandarasi waliokuwa eneo la mradi kushindwa kutoa majibu ya msingi kuhusu ucheleweshaji wa kazi, jambo lililosababisha kuitwa kwa viongozi wakuu wa kampuni hizo kutoka makao makuu yao nchini China.
Katika kikao hicho, kampuni mbalimbali zilifanya ahadi za kimaandishi kwa Serikali kuhusu ukamilishaji wa miradi. Miongoni mwao ni kampuni ya Shandong, inayotekeleza ujenzi wa miundombinu ya BRT kutoka Mwenge hadi Tegeta.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: