Rais Magufuli Ashtukiza Ubungo, Aahirisha Mbio za Mwenge
Автор: CHAMPION HABARI
Загружено: 2020-03-16
Просмотров: 38330
Описание:
RAIS John Pombe Magufuli, amesitisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2020 zilizotarajiwa kuanza hivi karibuni ili kuepuka maambukizi ya homa ya virusi vya Corona.
Ugonjwa huo uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 6,513 katika nchi mbalimbali duniani umeingia Afrika Mashariki katika nchi za Kenya, Rwanda.
Magufuli ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la njia za juu eneo la Ubungo linalounganisha barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela.
“Ninafahamu kitu kingine kinacholeta mkusanyiko ni Mwenge na tulitegemea kuwasha mwenge karibuni kule Zanzibar ambapo ungewezwa kutembezwa nchi nzima, hivyo nimeamua mbio za Mwenge hazitafanyika mpaka Corona iwe imeondoka,” amesema.
Ameongeza kwamba fedha za mbio za Mwenge zitatumika katika kujiandaa na tahadhari zaidi ya Corona ambayo imeshafika Kenya na Rwanda na kwamba hadi sasa hakuna mgonjwa wa homa hiyo nchini na baadaye mbio za Mwenge zitaendelea itakapothibitishwa ugonjwa huo umeisha duniani.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: