Hoja za Kishimba mapitio ya sera ya elimu; Waziri Mkenda aeleza kinachoenda kufanyika
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2022-09-26
Просмотров: 2150
Описание:
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa mfano wa miongoni mwa mambo watakayoyaangalia kwenye majadiliano ya mapitio ya sera ya elimu yaliyoanza leo Jumatatu Septemba 26 2022 ni maelekezo ya Rais Samia, ikiwemo hoja za Mbunge wa jimbo la Kahama Jumanne Kishimba bungeni ya mwanafunzi kumaliza limu ya juu akiwa hana stadi za maisha.
Majadiliano hayo yanafanyika kwa takriban siku 3 kuanzia leo Septemba 26 hadi Septemba 28 mwaka huu ukijumuisha wahadhiri, waajiri, wadau wa maendeleo, taasisi za umma na binafsi, taasisi za dini, taasisi za uendeshaji wa lugha, wabunge na timu ya Zanzibar inayoshughulikia sera na mitaala.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: