UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI KIBIASHARA I ANZA NA MTAJI MDOGO
Автор: Shamba hub
Загружено: 2025-05-25
Просмотров: 6449
Описание:
#kuku #kukuwakienyeji #chiken #hen
UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KIBIASHARA
Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni miongoni mwa shughuli zilizozoeleka katika jamii yetu. Hauhitaji gharama kubwa.
Unaweza kuanza na mitetea miwili na jogoo mmoja kulingana na ukubwa wa mtaji wako.
Mitetea yako ikianza kutaga kusanya mayai. Watakapotamia watamishie endapo haujui tafuta mtu atakaye kusaidia kutamishia kuku wako.
Wakitotoa watunze vifaranga vizuri. Idadi ya kuku zako itaongezeka kadri unavyozidi kutamishia kuku
JINSI YA KULEA VIFARANGA
Nunua pumba laini kwaajili ya vifaranga
Maji ya kunywa changanya na alovera kwa kukatia vipande vidogo kisha changanya wawekee kwenye chombo kisafi.
Maji hayo yenye alovera yatawakinga kuku na magonjwa nyemelezi.
Badilisha maji kila baada ya masaa 3 hadi 6
Usiwe na tamaa ya nyama za kuku wala mayai.
Kuwa na malengo thabiti kuwa baada ya muda fulani uwe na idadi kubwa ya kuku.
Ukifikia malengo anza kuuza kiasi kidogo cha mayai na baadhi ya kuku hasa majogoo ili ujiingizie kipato.
MFANO WA JINSI YA KUTAYARISHA CHAKULA CHA KUKU
1. Pumba ya mahindi 30kg
2. Mashudu ya alzeti 3kg
3. Cotton 2kg
4. Calcium 1kg
5. Dagaa 2kg
6. Polland 2kg
7. Paraza 3kg
8. Chokaa 1kg
9. Premix (robo)
JANE NNKO
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: