MTANZANIA aliyeunda Bajaji sasa kufungua kiwanda 'Nimepata nguvu'
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2018-09-06
Просмотров: 33858
Описание:
Mtanzania aliyeunda BAJAJI, Mzee Andrew Mbanga amesema anatarajia kufungua kiwanda cha kutengeneza chombo hicho kwa sababu amepata nguvu baada ya kukutana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage.
Akizungumza na Ayo Tv, Mzee Mbanga amesema kukutana na Waziri kumempa nguvu ya kufungua kiwanda chake ambapo awali alishindwa kwa sababu BAJAJI aliyounda ilikosa kibali.
"Amenipa nguvu na kufikiria nitengeneze kiwanda changu mwenyewe," amesema.
Amesema kuwa wazo la kuunda BAJAJI alilipata kutokana na sera ya Rais John Magufuli kuhusu uchumi wa viwanda, ambapo akaona na yeye atafute jambo la kuunga mkono sera hiyo.
"Nilijiuliza nitamuunga vipi mkono Rais wangu, nikasema lazima nifanye jambo ambapo nikafikiria kuunda Bajaji itakayoweza kuwabeba watu 6 ili kurahisha usafiri na kujiongezea kipato,"amesema.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: