ISSAH SAIDI MOHAMED AWACHARUA VIONGOZI WA CHADEMA BARA
Автор: BONGO CHANNEL TV
Загружено: 2026-03-05
Просмотров: 16
Описание:
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed amedai kuwa viongozi wa sasa wa Kitaifa wa chama hicho wakiongozwa na Tundu Lissu (Mwenyekiti Taifa), John Heche (Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara) na John Mnyika (Katibu Mkuu) ndio waliokuwa mstari wa mbele kuratibu njama ovu za kuihujumu Zanzibar ndani ya chama hicho
Anasema yeye na wenzake kutoka Zanzibar wamekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Zanzibar kwenye chama hicho kwa muda mrefu kupitia vikao rasmi vilivyokuwa vinaongozwa na Mwenyekiti Mstaafu wa Taifa Freeman Mbowe, lakini 'kundi la Lissu, Heche na Mnyika' ndilo lililokuwa kikwazo, ingawa Mbowe alikuwa anaonesha mwelekeo wa kushughulikia changamoto hizo
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Machi 05.2026, Said Issa Mohamed pia amekanusha madai ya kwamba yeye alishindwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika mwanzoni mwa mwaka 2025, badala yake aliamua kujiondoa kwenye 'round ya pili' kutokana na kwamba 'alinusa harufu' ya kuwa na uongozi usiothamini nafasi ya Zanzibar chini ya Lissu, kwakuwa anawajuwa watu hao tangu awali walipokuwa wakivutana kwenye vikao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: