CLOUDSFM wachambua na kutaja sababu na chokochoko ndani ya Simba hali ni mbaya kwa viongozi
Автор: banyaleotv
Загружено: 2026-02-06
Просмотров: 440
Описание:
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema hana mpango wa kuachia nafasi yake ya uongozi licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili klabu hiyo kwa sasa.
Mangungu ameeleza kuwa anaendelea kushika wadhifa huo kwa sababu wanachama na viongozi waliompa dhamana ya kuiongoza Simba bado wanamuamini na wanampa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.
Amesema akiwa kama kiongozi, anatambua uwepo wa changamoto ndani ya klabu, lakini ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Simba inazidi kupiga hatua na kurejesha mafanikio yaliyotarajiwa na mashabiki pamoja na wanachama wa klabu hiyo.
Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kuitisha mkutano na kutoa maneno ya kashfa na kauli zisizo na staha kwa Mwekezaji wa Simba, Ndugu Mohammed G. Dewji. Vitendo hivyo visivyo vya kiungwana, havikubaliki. Uongozi wa Klabu unatoa pole kwa Ndugu Mohammed Dewji.
Aidha, uongozi wa Klabu umeliandikia Jeshi la Polisi kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote waliohusika katika mkutano huo ama kula njama na kuwafikisha katika vyombo vya dola kwa makosa ya jinai.
Bodi inasisitiza kuwa haitabariki wala kuvumilia mtu yeyote atakayeiharibu taswira ya Klabu kwa namna yoyote ile.
#mgogorosimba
#shidandaniyasimba
#simbatatizo
#banyaleotv
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: