MWILI WA ANAYETAJWA KUJINYONGA KITUO CHA POLISI ULIVYOZUNGUSHWA MOSHI
Автор: TZA MEDIA HUB
Загружено: 2026-01-19
Просмотров: 19
Описание:
Jumamosi ya Januari 17, 2026, kabla hata ya jeneza kushushwa kaburini, Moshi ilishuhudia tukio lisilo la kawaida. Gari maalumu lililobeba mwili wa kijana Michael Rambau (18) lilipotoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC ambako mwili huo ulikuwa umehifadhiwa, lilikutana na msururu mrefu wa pikipiki na bajaji, uliogeuka kuwa maandamano ya kimya lakini yenye ujumbe mzito.
Msafara huo, uliohusisha mamia ya vijana wengi wao wakiwa ni madereva wa bodaboda na bajaji, ulizungushwa katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Moshi, huku milio ya honi na injini za pikipiki ikisikika kila kona. Safari hiyo ilihitimishwa nyumbani kwa marehemu, mtaa wa Karikacha, Kata ya Rau, ambako shughuli za maziko zilifanyika.
Michael Rambau, aliyekuwa fundi bomba na dereva wa bodaboda, anadaiwa kufariki dunia Januari 13, 2026 baada ya kujinyonga kwa kutumia mkanda akiwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Moshi, kwa mujibu wa Jeshi la Polisi.
Hata hivyo, mazingira ya kifo chake yameibua sintofahamu kubwa, huku zaidi ya maswali 10 tata yakitajwa bado hayajapata majibu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, marehemu alikamatwa Januari 13 kwa tuhuma za kumshambulia baba yake mdogo, Brian Felix, kwa kumpigia bapa la panga. Kamanda Maigwa amesema akiwa mahabusu, mtuhumiwa huyo alidaiwa kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia mkanda.
Katika taarifa iliyotolewa Januari 14, 2026, Polisi walieleza pia kuwa awali Michael alikuwa anatuhumiwa kuhusika katika tukio la kumjeruhi baba yake mzazi mnamo Novemba 25, 2025, kwa kumchoma shingoni kwa kitu chenye ncha kali, kabla ya kutoroka na kukamatwa baadaye Januari 13 mwaka huu.
“Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kubaini mazingira kamili ya kifo cha kijana huyo akiwa mahabusu,” amesema Kamanda Maigwa, akisisitiza kuwa uchunguzi huo unazingatia taratibu zote za kisheria.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: