MGOMBEA UBUNGE HANDENI AAHIDI KUSAKA SOKO LA KUKU
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-09-08
Просмотров: 376
Описание:
Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Jimbo la Handeni mkoani Tanga, Mhandisi Charles Sungura, amewaahidi wananchi wa eneo hilo kuwa endapo watamchagua, atawatafutia soko la uhakika la kuuza kuku, kwani wapo wengi, ila wamekosa soko la uhakika.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni zake zilizofanyika katika Kata ya Mkata, wilayani Handeni, leo Jumatatu, Septemba 8, 2025, Charles amesema wilaya hiyo inazalisha kuku wengi, hivyo uzalishaji huo unatakiwa uwe na faida kwa wananchi.
Ameahidi kuwatafutia wananchi hao mashine za kutotolesha mayai, lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha kila anayefuga kuku kwenye kata anaona faida ya ufugaji.
Mhandisi Mwanaisha Ulenge, mgombea ubunge mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, kwa upande wake, amewashukuru wanawake wa Handeni kwa kumchagua tena, na kuahidi kwenda kushirikiana nao kuleta maendeleo katika yale ambayo tayari walianza kuyafanya.
Video na Rajabu Athumani
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: