ASHANGAZWA MKOPO WA10% ULIVYOPOTEA PAMOJA NA MAJINA KUTOKA/MJASIRIAMALI ANAESAIDIA YATIMA NA VIJANA
Автор: WEMU ONLINE TV
Загружено: 2026-03-10
Просмотров: 16
Описание:
Mjasiriamali mama Erica Mashoko mkazi wa Mombasa Jijini Dar Es Salaam amesimulia changamoto anazopambana nazo katika biashara yake ya kuuza malighafi ya kutengeneza chakula cha kuku kwa njia ya damu ya ng'ombe anayoipata katika machinjio ya Mazizini.
Mama huyo amesema katika biashara hiyo inamsaidia kipato kidogo ambacho anasomesha watoto wake pamoja na watoto yatima.
Amesema mbali na yatima katika biashara yake hiyo ndogo pamoja na changamoto ameweza kuajiri vijana na kuwaondoa kwenye athari za kujiunga na makundi ya vijiweni na kuvuta bangi.
Mama Mashoko anasema mtaji wake ni mdogo kiasi kwamba anatamani apate mtaji mkubwa walau atanue biashara yake ili pia aweze kuajiri vijana zaidi.
Aidha katika harakati za kutafuta mkopo ameshangaa Ile mikopo ya asilimia kumi hakufanikiwa kupata mpaka leo pamoja na kuelekezwa kuandika katiba ambapo walipokamilisha waliiwasilisha sehemu hisika na majina yakatoka lakini mpaka leo hajafanikiwa kupata mkopo huo wa asilimia 10.
##
#
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: