WANAKIJIJI WASHAMBULIWA NA KUPIGWA NA WALINZI WA MWEKEZAJI HUKO VIKINDU NA KUHARIBIWA MAZAO YAO.
Автор: KAHITILA 255
Загружено: 2025-06-13
Просмотров: 1021
Описание:
Baadhi ya Wanakijiji kutoka kijiji cha kazole kusini, Kata ya Vikindu, Wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani wamelalamia kuharibiwa mazao na kupigwa na Watu wanaodaiwa kuwa Walinzi wa mwekezaji katika eneo hilo.
Awali eneo hilo linadaiwa kuwa lilikuwa chini ya umilikiwa wa Mwekezaji ambae alipanga kufanya uwekezaji wa Kiwanda miaka ya nyuma lakini akashindwa kuliendeleza.
Wanakijiji hao wanadai kuruhusiwa kuendesha shughuli za Kilimo katika eneo hilo lililoko katika Kijiji cha Kazole Kusini ndani ya Wilaya ya Mkuranga na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt John Magufuli baada ya kumlalamikia kwamba eneo hilo lilikuwa msitu na Pori kubwa.
Amini Japhet, Mpati Mbalawa pamoja na Nuru Mbonde ni baadhi ya Wananchi wa Kijiji hicho ambao wamedai kushambuliwa na Watu wanaodaiwa kuwa Walinzi wa eneo hilo.
#kahitila255
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: