BILIONI MIA TANO KUKARABATI MGR
Автор: TRC RELI TV
Загружено: 2026-02-02
Просмотров: 1067
Описание:
Je wajua
Unajua TRC inaendelea na uboreshaji wa reli ya zamani (MGR)
Shirika la reli Tanzania (TRC) kwa ushirikiano na Bank ya Dunia inatumia shilingi Bilioni mia tano (500) kufanya ukarabati mkubwa wa Reli ya MGR kutoka Dar es Salaam hadi Bandari kavu ya Isaka jumla ya kilomita 292.
Reli za pound 60 ambazo ni za kizamani zinatolewa na kuwekwa reli za pound 80, reli hizi za pound 80 zitaongeza kasi ya treni mara mbili zaidi ya reli ya pound 60 ambayo treni inakwenda kwa kasi ya km 30-40 kwa saa, baada ya mabadiliko haya treni itakwenda kwa kasi ya kilomete 70 kwa saa.
Maboresho hayo mbali na kuongeza kasi ya treni yatawezesha treni kubeba tani 18 na nusu kwa exal tofauti na reli pound 60 inayobeba tani 15 kwa exal.
Kwa hakika ukarabati huu utawezesha treni kubeba mzigo mzito na kufika kwa haraka, kwa sasa treni inavuta mabehewa 20 baada ya ukarabati treni itavuta mabehewa 40.
Ili kuhakikisha treni zinapishana vizuri njia za kupishana kwa sasa zina urefu wa mita 400 zitaongezwa na kuwa mita 650.
Katika uboreshaji huu kutajengwa madaraja tatribani 171 kuanzia Dar es Salaam hadi Isaka na kujenga mabwawa sita eneo la kinyasungwe ili kudhibiti mafuriko yanayoharibu reli eneo la kilosa gulwe.
Mradi umeanza mwezi March, 2025 na unatarajiwa kukamilika Disemba, 2029.
Huu ni mradi mkubwa wananchi wanapatiwa elimu ya uelewa wa mradi ili kutoa ushirikiano kwa wakandarasi.
Reli yetu ,maendeleo yetu, Taifa letu, kazi iendelee.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: