ROAD2RECOVERY; UAMUZI WA KUKOMBOA & KUMILIKI KILICHO CHAKO
Автор: Adamhajj ministries official
Загружено: 2021-10-04
Просмотров: 14922
Описание:
REV. DR. ADAMHAJJ asisitiza zaidi na kufafanua kwa undani ya kwamba kwa kila jambo au hoja kutimizwa linahitaji uamuzi.Twahitaji kupindua hali ya uchoyo, hali ya kuishi katika ubinafsi maishani mwetu. Hakuna kitakachobadilika katika ulimwengu wetu hadi pale kila mmoja wetu atakapokuwa radhi kubadilika. Mara nyingi huwa tunatamani ulimwengu ubadilike bila ya kukoma kutambua kwamba hali ilivyo ulimwenguni
inatokana na njia tunazoishi katika maisha ya ubinafsi na chaguo
tunalofanya kila siku. Ikiwa kila mmoja hapa duniani anafahamu jinsi ya kupokea na kuonyesha upendo, dunia yetu ingelikuwa mahali tofauti kabisa
pa kuishi. Nafikiri sote twafahamu kuwa kuna jambo lililo kasoro
katika jamii na kwamba lahitaji kutatuliwa. Lakini hakuna mtu
anayefahamu kinachopaswa kufanywa au jinsi ya kuanza kufanya
mabadiliko. Jibu letu kwa ulimwengu usioweza kuthibitika ni
kulalamika na kufikiri, kuna mtu anayepaswa kufanya jambo fulani.
Tunafikiri na kusema kuwa pengine Mungu au serikali au mtu
mwingine yeyote aliye kwenye mamlaka anahitajika kufanya
kitendo. Lakini ukweli ni kwamba kila mmoja wetu anahitajika
kufanya jambo fulani. Lazima tujifunze kuishi maisha yenye
mwelekeo tofauti kabisa na tulivyo sasa. Lazima tuwe radhi
kujifunza, kubadilika na kukubali kwamba sisi ni sehemu ya tatizo
lililoko.
Hatuwezi kutatua kile tusichoelewa, kwa hiyo hitaji letu la
kwanza ni kutafuta chanzo cha tatizo lililoko. Ni kwanini watu
wengi hawana furaha? Ni kwanini ghasia zimeongezeka sana katika
familia, maeneo jirani, miji na mataifa?
REV. DR. ADAMHAJJ MINISTRIES
For Support & Tithe : +254700146495
WATSUP : +254777700486
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: