KAULI YA KWANZA YA LUCY KOMBANI BAADA YA USHINDI UBUNGE VITI MAALUM MOROGORO
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-07-30
Просмотров: 2206
Описание:
Mchakato wa kura za maoni kuwapata wagombea ubunge viti maalumu kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani Morogoro umekamilika, huku Lucy Kombani akiongoza kwa kupata kura 1,314 kati ya kura halali 1,646 zilizopigwa, akifuatiwa na Sheila Lukuba aliyepata kura 597.
Katika mkutano huo maalumu wa kura za maoni, jumla ya wajumbe 1,653 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, kura 6 zimeharibika na kufanya kura halali kuwa 1,646.
Akitangaza matokeo jana Jumatano Julai 30, 2025 saa tano usiku, Msimamizi wa uchaguzi huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema shughuli hiyo imehusisha wagombea tisa akiwemo Josephine Kupuna aliyepata kura 454, Jane Claude Mihanji 339, Aliyah Awadh Omar 236, Amina Ally Karuma 153, Hajira Said Mwikoko 90, Kulwa Nuhu Kangeta 75 na Rahel Mashishanga 37.
“Niwapongeze wajumbe kwa hatua hii nzuri tuliyofikia baada ya hapa majina yanaenda ngazi za juu kwaajili ya taratibu za mwisho kwa mujibu wa taratibu za chama chetu cha Mapinduzi,” amesema Malima.
Naye Lucy Kombani amewashukuru wasimamizi kwa kusimamia upigaji kura wajumbe wote kupiga kura kwa uhuru na haki, huku akiahidi kuunga mkono mipango ya Serikali kwa maslahi mapana ya Watanzania na Taifa kwa ujumla.
Mkutano huo maalumu wa UWT Mkoa wa Morogoro umefanyika katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Xxx
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: