HUKU ESTER BULAYA KULE MSUKUMA BUNDA LEO ILIKUWA NONDO TUPU.
Автор: KAHITILA 255
Загружено: 2025-09-13
Просмотров: 742
Описание:
Mgombea Ubunge wa jimbo la Bunda mjini, lililopo Mkoani Mara, Ester Bulaya amewaahidi wananchi katika jimbo hilo pindi watakapomchagua atahakikisha anasimamia ujenzi wa Barabara za mitaa kwa kilomita 25 Pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi.
Bulaya ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi katika jimbo hilo ambao umefanyika katika stendi ya zamani ya mabasi .
Bulaya amesema kwasasa wananchi wanahitaji kuona mji wa Bunda unakuwa na hadhi kama lilivyo jina lake hivyo atakapoingia bungeni atahakikisha barabara za mitaa, soko pamoja na stendi zinajengwa kisasa.
Kwa upande wake Mgombea ubunge wa jimbo la Geita Vijijini Joseph Musukuma, amesema kuwa Ester Bulaya ni miongoni mwa watu makini katika kuchangia hoja zenye kuleta maendeleo Bungeni hivyo amewaomba wananchi hao kumchagua kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la hilo.
#kahitila255 #bunda #ccm
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: