21 February 2026
Автор: AFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA
Загружено: 2026-02-21
Просмотров: 14
Описание:
MAFUZO YA UANDISHI WA WA SHERIA
Mkurugenzi wa Mashtaka Mhe. Mgeni Jailani Jecha Amewataka wanasheria katika taasisi za serikali kuzifanyia kazi sheria ambazo zina mapungufu na zilizopitwa na wakati ili kuleta tija katika utendaji wa kazi zao.
Ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya uandishi wa uwandishi wa sheria kwa wanasheria kutoka taasisi mbalimbali za serikali huko katika Kituo cha mafunzo ya sheria na utafitii kilichopo Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B.
Amesema taasisi nyingi za serikali zimekua zikipambana na changamoto za kiutendaji katika mausala ya kisheria kutokana na sheria hizo kupitwa na wakati.
Mkuu wa kituo cha mafunzo ya sheria na Utafiti Zanzibar Ali Hilali Vuai amewaomba wataalamu hao wa sheria kuyatumia mafunzo hayo katika kuendeleza fani ya sheria ili kuleta tija kwa serikali na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo ya muda mfupi Kutoka kituo cha mafunzo ya sheria na utafiti Zanzibar Jina Mwinyi Waziri amesema mafunzo hayo yanalenga kuisaidia serikali kupata wanasheria watakaokua na uwelewa katika uwandishi wa miswada wa kisheria.
Nao washiriki wa Mafunzo hayo wameahidi kuyafanyika kazi mafunzo hayo kwa kuandika miswada kitaalamu na kuleta mabadiliko katika taasisi zao.
Jumla ya washiriki 11 kutoka taasisi mbalimbali za serikali walishiriki mafunzo hayo ambayo yaliendeshwa kwa muda wa siku 15 ikiwa ni muendelezo wa Mafunzo yanayotolewa katika kituo cha Mafunzo ya Sheria na Utafiti Zanzibar.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: