Mtu mmoja anazuiliwa kwa kumuuwa mamake wa miaka 100 Kericho
Автор: Citizen TV Kenya
Загружено: 2026-03-10
Просмотров: 1048
Описание:
Mwanaume mmoja anayeshukiwa kumuua mama yake mwenye umri wa miaka 100 katika Kaunti ya Kericho, amefikishwa mahakamani. Julius Cheruiyot Bett alifikishwa mahakamani Jumatatu, kuhusiana na kifo cha mama yake, Grace Chelangat Chepkwony.
Mahakama ya Kericho iliamuru mshukiwa azuiliwe katika kituo cha polisi cha Sondu kwa siku nane ili kuwapa wapelelezi nafasi ya kukamilisha uchunguzi kuhusu tukio hilo. Kwa mujibu wa familia na mashahidi mshukiwa anadaiwa kuchukua gari la dadake lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba ya mama yake na kumgonga mama huyo mzee na kumjeruhi vibaya.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: