Kesi ya kina MDEE yaahirishwa tena
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2022-10-13
Просмотров: 233
Описание:
Dar es Salaam. Mbunge wa viti maalim ambaye ni mmoja wa wabunge viti maalim 19 waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega ameieleza mahakama alifukuzwa uanachama bila kupewa haki ya kusikilizwa.
Tendega ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema(Bawacha) ametoa maelezo hayo mahakamani leo Alhamis, Oktoba 13, 2022, wakati akihitimisha ushahidi wake katika kesi yao ya kupinga kufukuzwa uanachama wa chama hicho.
Wabunge hao akiwemo Halima Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: