CUF KWAZIDI KUFUKUTA, POLISI YAWATOA VIGOGO KIKAONI
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2026-02-20
Просмотров: 790
Описание:
Mjumbe wa Baraza la Chama cha Wananchi (CUF), Mohammed Ngulangwa, pamoja na wenzake wawili, wamejikuta wakishikiliwa na Jeshi la Polisi na kutolewa nje ya kikao kinachoendelea cha baraza la chama hicho, ambacho kilikuwa kikijadili majina ya wagombea watakaoingia katika kinyang’anyiro cha nafasi za juu ndani ya chama.
Sababu ya kuondolewa kwao katika kikao hicho, kilichogubikwa na kelele, makonzi na misukosuko ya hapa na pale, ni madai kwamba walikuwa wakipinga kila hoja iliyowasilishwa, jambo lililodaiwa kuwanyima wajumbe wengine utulivu.
Kikao hicho kinaendelea katika makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam. Ikumbukwe kuwa Ngulangwa na wenzake ni wafuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba, na msimamo wao ni kwenda Mahakamani kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa wa kutengua uchaguzi uliomweka madarakani uongozi mpya wa chama.
Awali, Mwananchi ilizungumza na Ngulangwa na kumuuliza sababu za kushiriki kikao hicho ilhali msimamo wao haukubaliani na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa. Katika majibu yake alisema: “Huwezi kupinga jambo ukiwa nje ya mchakato. Naenda kushiriki ili niweze kupinga uamuzi utakaofikiwa,” amesema.
Endelea kufuatilia Mwananchi
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: