#UDSMLive
Автор: Mkwawa University
Загружено: 2022-11-22
Просмотров: 439
Описание:
Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa Profesa Esther William Dungumaro anayo furaha kuwaalika wadau wote wa Elimu na wananchi kwa ujumla kwenye Mahafali ya 14 ya Chuo yatakayofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Chuo siku ya Jumatano tarehe 23 Novemba 2022 kuanzia saa moja na nusu asubuhi. Mgeni Rasmi kwenye Mahafali hayo ni Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Nyote mnakaribishwa.
Vilevile, mnataarifiwa kwamba mahafali hayo yatarushwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa, youtube - kwa jina la ’Mkwawa University’; Instagram – kwa jina la ’Mkwawa_University_College’, Twitter and Facebook kwa jina la ’MUCE_yetu’.
#MUCE
#Mkwawa
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: