Makambi - Tehillah Singers Tz
Автор: Tehillah Singers Tz
Загружено: 2024-06-21
Просмотров: 875
Описание:
Sikukuu hii ya vibanda ilikuwa inafanyika tarehe 15 mwezi wa 7 kila mwaka. Mambo ya Walawi 23:33-34 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana.
Sikukuu hii ilikuwa inawataka watu wote hata kama sio Waisrael basi wahudhurie, maana kulikuwa na Baraka zilizopatikana kwa waliokuwa wakihudhuria sikukuu hii ya Makambi, na wale wasiohudhuria kuna mabaya yalikuwa yanawakuta: Zekaria 14:16-18 Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, na kuishika sikukuu ya Vibanda.Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo Bwana atawapiga mataifa, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.
Kwa hiyo sikukuu hii ya vibanda ilikuwa inasherekewa baada ya watu kuvuna mavuno yao, na kutoa sadaka ya malimbuko, ndipo watu walitoka majumani mwao na kwenda mbali na makazi yao, kisha walijenga Vibada na kukaa huko kwa siku 7. Mambo ya Walawi 23:42 Mtakaa katika vibanda muda wa siku saba; wazalia wote wa Israeli watakaa katika vibanda;
Hata Yesu alipokuwa hapa Duniani alisherekea sikukuu hii ya vibanda: Yohana 7:2-10 Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya….Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo.Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu… Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.
LENGO KUBWA LA KUSHEREKEA SIKUKUU YA VIBANDA:
1. Sikukuu hii ilikuwa inawakubusha Israel kwamba wao walikuwa watumwa katika nchi ya Misri, Mambo ya Walawi 23:42-43
Kwa sasa tuasherekea sikukuu ya vibanda kama ishara ya kukombolewa kutoka katika Misri (utumwa) wa Dhambi, maana dhambi ni Utumwa Yohana 8:34-35 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
2. Sikukuu ya vibanda kwa Waisraeli iikuwa ni kujifunza Historia ya ukombozi kutoka Misri kuelekea Nchi ya Kanani, Hivyo watu walikutanika kwa lengo la kujifunza Mambo ya Mungu kwa Siku 7, Walionyana, na kutiana moyo, na kufahamiana kwa wale waliokuwa wanaishi mbali: Kumbukumbu la Torati 31:9-11
Kwa sasa lengo la kusherekea pia sikukuu ya vibanda ni kujifunza Historia ya Ukombozi, na jinsi Mungu alivyotukomboa kutoka katika Utumwa wa Dhambi, na hivyo Tunaonyana pale penye mapungufu na kutiana moyo pale tulipoimarika: Waebrania 10:24-25 "tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia"
.Tunaona hata Yesu alipohudhuria sikukuu ya Vibanda alienda kuwafundisha watu Neno la Mungu: Yohana 7:14-15 Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha.Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma?
3. Sikukuu ya vibanda iliwakumbusha Waisraeli kwamba wao ni wapitaji tu katika Jangwa bali makao yao ya ahadi ni Kanani ambayo Mungu alikuwa amewaandalia, Ndivyo ilivyo kwa sasa tunaposherekea sikukuu ya Vibanda, kwa kuacha shughuli na nyumba zetu, inatukumbusha kwamba sisi hapa Duniani ni wapitaji na wasafiri tu, bali makao Yetu ya Milele ni katika Kanani ya Mbinguni(Yerusalemu). 1 Petro 2:11
4. Israel Kabla ya Kuingia Kanani walikuwa hawana Makao ya kudumu kule jangwani ,Na hivyo walikuwa wanaishi katika mahema tu, na sikukuu ya Vibanda iliwakumbusha kwamba hayo sio makao yao ya kudumu, bali yapo makao maalumu, Hii inatukumbusha pia tunaposherekea sikukuu ya makambi ni kwamba hata nasi kabla ya kuanza kuishi katika Yerusalemu mpya, Tutaishi katika kambi kwanza na tutakuwa wageni Ufunuo wa Yohana 20:9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
Na baada ya kuishi katika kambi ndipo Watakatifu wataishi katika Yerusalemu mpya makao ya milele: Ufunuo wa Yohana 21:2-3 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: