WAKILI MWAMBUKUSI AIBUA YA OKTOBA 29 MAKAMU WA RAIS AMJIBU TUSITONESHANE
Автор: MIMI ONLINE TV
Загружено: 2026-02-02
Просмотров: 21
Описание:
Makamu wa Rais Dk Emmanuel Nchimbi amesema kitendo cha baadhi ya viongozi wa Serikali, taasisi za kijamii, vyama vya siasa na wanaharakati kuendelea kuzungumzia yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, nje ya mfumo wa kisheria uliowekwa juu ya jambo hilo, ni kutotendea haki taifa.
Dk Nchimbi amesema hayo leo Februari 2, 2026, alipozungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Sheria na kuanza kwa mwaka wa Mahakama 2026 jijini Dodoma, akiwa mgeni rasmi.
Makamu huyo wa Rais ametoa kauli hiyo akijibu ombi lililotolewa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, aliyesema TLS inatambua yaliyojitokeza kabla, wakati na baada ya uchaguzi, na kwamba wanapendekeza kila anayehitajika kuwajibika awajibike kwa maslahi mapana ya taifa.
#samiasuluhuhassan #tanzania #wazirimkuu #mwigulunchemba #raissamia
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: