Zahabu na feza haziniokoi ( 5 NW)
Автор: Shem Kabanza
Загружено: 2020-05-12
Просмотров: 50973
Описание:
https://www.nyimbozawokovu.online/5-d...
Zahabu na feza haziniokoi ( 5 NW)
Nyimbo Za Wokovu
1. Dhahabu na fedha haziniokoi,
Hazina na mali haziponyi roho,
Lakini kwa damu ya Yesu mwokozi
nimenunuliwa nipate uhuru.
Refrain :
Nimekombozwa pasipo mali,
kwa neema nimeokoka !
Ni bei ghali : kwa damu yake
Alilipa deni langu.
2. Dhahabu na fedha hazinilipii
madeni makubwa ninayo kwa Mungu.
Mwokozi alinikomboa kwa damu
nipate wokovu, nitoke dhambini
3. Dhahabu na fedha haziufungui
Mlango wa ku’karibia mwenyezi,
Lakini kwa damu nimeifikia
Neema ya Mungu aliya mkuu.
4. Dhahabu na fedha hazinifikishi
nyumbani mwa Mungu niliyemwasia,
Lakini nimekombolewa kwa damu,
kwa hiyo nitachukuliwa mbinguni.
#Nyimbozawokovu
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: