NELICO YAKUTANISHA VIONGOZI WA DINI KUJADILI AMANI KUELEKEA UCHAGUZI
Автор: Saa 24
Загружено: 2025-10-06
Просмотров: 1
Описание:
Shirika lisilo la kiserikali la Nelico, lenye makao yake makuu mkoani Geita, limeendelea kuendesha midahalo mbalimbali ya kuhimiza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mdahalo huo umefanyika mjini Geita, na umewakutanisha viongozi wa dini mbalimbali kutoka mkoani humo, ambapo wamehimiza wananchi kuepuka vitendo au viashiria vyovyote vinavyoweza kuvunja amani ya nchi.
Katika mada kuu ya mjadala huo, viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa viongozi wa dini kuhubiri amani katika kipindi cha uchaguzi, wakisema nyumba za ibada zina nafasi kubwa katika kuimarisha umoja wa kitaifa.
#saa24 #UchaguziMkuu2025
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: