Breaking News : WATU 6 WAKAMATWA KWA KUUA NA KUNYOFOA SEHEMU ZA SIRI ZA MAITI MANYONI
Автор: WazoHuru Media
Загружено: 2023-03-28
Просмотров: 5160
Описание:
Jeshi la Polisi Mkoani Singida Kupitia Misako Mbalimbali kuanzia Machi 16 Mwaka huu limefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa Sita Wanaojihusisha na Matukio ya Mauaji na kufukua Makaburi katika Wilaya ya Manyoni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani hapa Kamanda wa Polisi ACP Stella Mutabihirwa Amesema Watuhumiwa hao Wamekiri Kuhusika na Matukio hayo huku Akibainisha kuwa Matukio hayo yanahusishwa na Imani Za Kishirikina.
Aidha Kamanda ACP Mutabihirwa ametoa wito kwa wananchi Mkoa wa Singida hasa wakazi wa Wilaya ya Manyoni ambako Vitendo hivyo vimeshamiri,Kuachana na imani Potofu za Kishirikina za Kutafuta Utajiri kwa njia za kishirikina.
Baadhi ya Wananchi wa Manyoni wameishukuru serikali kwa hatua hiyo ya kukamata wahalifu wanaojihusisha na mauaji na kwamba sasa watakaa kwa amani hivi sasa.
CC @hamisihussein_tz
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: