TAZAMA JINSI DARAJA LA SUNGWE LILIVYOBORESHA USAFIRI KATIKA BARABARA YA TANZAM, WANANCHI WAFUNGUKA
Загружено: 2026-01-22
Просмотров: 679
Описание:
Ujumbe wa wataalam kutoka TANROADS Makao Makuu kupitia Kitengo cha Ushauri wa Kihandisi (TECU), kwa kushirikiana na TANROADS Mkoa wa Mbeya, umefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Sungwe lililopo katika barabara ya TANZAM mkoani Mbeya na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu pamoja na thamani ya fedha zilizotumika.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, amesema daraja hilo limejengwa kufuatia madhara makubwa yaliyosababishwa na Kimbunga Hidaya pamoja na mvua kubwa za El Niño, ambazo zilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu katika eneo hilo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: