WAJENZI WA TAIFA-SHABAAN ROBERT 01
Автор: PHILLIP BUGOBORA
Загружено: 2022-04-05
Просмотров: 108
Описание:
Mwalimu Nyerere alivutiwa sana na umahiri wa Shaaban Robert hata katika upande wa ushairi uliotukuka. Hadi sasa wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanasema tangu Shaaban Robert afariki tarehe 20 june, 1962 hakujatokea mtu yeyote aliekitendea haki Kiswahili kama alivyofanya Shaaban Robert katika uhai wake.
Shaaban alitoa mchango mkubwa katika taifa kwani katika uhai wake baada ya kumaliza darasa la 11 aliajiriwa na Serikali ya kikoloni wakati huo ikiitwa Tanganyika akiwa karani. Kuanzia mwaka 1926 mpaka 1944 alikuwa afisa forodha katika bandari mbalimbali nchini hasa Pangani na Bagamoyo, kuanzia mwaka 1944 mpaka 1946 alihamia mjini Morogoro katika ofisi ya mbuga za wanyama. Na kuanzia mwaka 1946 mpaka 1952 alihamia Tanga katika ofisi ya kupima ramani alipostaafu utumishi wa umma.
Shaaban Robert aliandika vitabu 24 kwa lugha adhimu ya kiswahili, na mpaka sasa kazi zake zinazidi kukusanywa na taasisi ya uchunguzi na kukuza Kiswahili (TUKI) ya chuo kikuu cha Dar es Salaam
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: