SERIKALI YAWAHIMIZA VIJANA RUKWA KUTUMIA FURSA ZA MISITU KUBORESHA AJIRA
Автор: Kakwale TV
Загружено: 2025-12-19
Просмотров: 40
Описание:
SERIKALI YAWAHIMIZA VIJANA RUKWA KUTUMIA FURSA ZA MISITU KUBORESHA AJIRA
Katika juhudi za Serikali kutatua changamoto ya ajira kwa vijana, wananchi mkoani Rukwa wametakiwa kutumia ipasavyo fursa zitokanazo na mazao ya misitu, hususan ufugaji wa nyuki, kama njia ya kujiongezea kipato na kujiajiri.
Wito huo umetolewa na Afisa Nyuki katika shamba la miti Mbizi lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, bi Emeliana Joseph Makang’a, ambaye ameeleza kuwa msitu huo una faida nyingi kupitia mazao mbalimbali yanayopatikana ikiwemo asali na nta.
Amefafanua kuwa kwa mwaka 2025, Serikali imefanikiwa kugawa zaidi ya mizinga ya nyuki 160 kwa wananchi ili kuwahamasisha kujikita katika shughuli za ufugaji nyuki.
Kwa upande wake, Lucas Kivuyo, Mhifadhi Daraja la Pili, amesema Msitu wa Mbizi wenye ukubwa wa hekta 23,427, ambapo hekta 2,605 kati ya hizo tayari zimepandwa miti kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya baadaye.
Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027, Msitu wa Mbizi unatarajia kuanza kuvuna miti kwa ajili ya uzalishaji wa mbao pamoja na nguzo zitakazotumika katika huduma ya umeme, hatua inayotarajiwa kuongeza mapato na fursa za ajira kwa wananchi wa eneo hilo.
SUBSCRIBE channel hii kupata habari kubwa zinazobamba mtandaoni / @kakwaletv
Like us on Facebook,
/ kakwaletvtz
Follow us on Twitter,
/ kakwaletv
Follow us on Instagram,
/ kakwaletv
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: