BPRA USO KWA USO NA WAJASIRIAMALI ZANIZBAR
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-19
Просмотров: 146
Описание:
Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) leo umefanya mafunzo kwa wajasiriamali wadogo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kusajili biashara zao ili iwe chachu ya kuwaletea maendeleo endelevu.
Mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wajasiriamali kuhusu umuhimu wa kusajili biashara zao kisheria, faida za kuwa na nyaraka halali za biashara pamoja na fursa zinazopatikana baada ya usajili ikiwemo kupata mikopo, zabuni na kushiriki kikamilifu katika uchumi rasmi.
Aidha, washiriki wamepata maelekezo ya kina kuhusu taratibu za usajili, matumizi ya mifumo ya kidijitali pamoja na haki na wajibu wao kama wafanyabiashara waliosajiliwa.
BPRA imeeleza kuwa itaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara ili kuhakikisha sekta ya ujasiriamali inakua na kuchangia ipasavyo katika maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.
#BPRA #Wajasiriamali #UsajiliWaBiashara #MaendeleoEndelevu #Zanzibar
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: