Usimamizi Endelevu wa Misitu na Ushirikiano na Jamii
Автор: Mazingira TV
Загружено: 2025-09-16
Просмотров: 30
Описание:
Mradi wa Mbinu Jumuishi za Maboresho ya Mnyororo wa Thamani wa Nishati Miti Nchini, unaotekelezwa na LEAT kwa kushirikiana na WWF Tanzania na Mpingo Conservation, Umehamasisha mafunzo kwa wahifadhi wa TFS wanaosimamia ugani na uenezi kutoka TFS Makao Makuu, kanda ya Mashariki, Kaskazini, Magharibi na kanda ya Ziwa ambapo mradi huu unatekelezwa. Katika mafunzo haya, washiriki wanajifunza kuhusu:
i. Usimamizi Endelevu wa Misitu: Mbinu bora za utunzaji wa misitu na njia za kudhibiti ukataji holela wa miti.
ii. Mbinu za Ufuatiliaji na Udhibiti wa Rasilimali za Misitu: Matumizi ya teknolojia na takwimu katika kufuatilia na kulinda misitu yetu.
iii. Msaada wa Ugani kwa Jamii Zinazotegemea Misitu: Kuimarisha uhusiano kati ya wadau wa sekta ya misitu na jamii zinazotegemea misitu kwa maisha yao.
iv. Haki za Binadamu na Utekelezaji wa Sheria: Kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sheria za misitu unazingatia haki za wananchi na unaleta maendeleo shirikishi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: