KAWE MAMBO YAMEPAMBA MOTO, UZINDUZI KAMPENI CCM SHAMRASHAMRA ZIMEANZA
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-08-28
Просмотров: 23286
Описание:
Burudani na shamrashamra zimetawala kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) zinazofanyika leo Agosti 28, 2025.
Mamia ya wananchi na makada wa chama hicho waliovaa sare za kijani na njano wanaendelea kuwasili uwanjani hapa kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa kampeni kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Katika mkutano huu, mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea mwenza, Dk Emmanuel Nchimbi wanatarajiwa kutambulishwa kwa Watanzania kabla ya kuendelea na kampeni katika mikoa mbalimbali nchini.
Wagombea hao ni miongoni mwa 17 walioteuliwa na INEC jana Agosti 27, 2025 kwa ajili ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Wagombea hao na vyama vyao watakwenda kwa Watanzania kunadi sera zao ili wawapatie ridhaa ya kuongoza Serikali katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: