ASKOFU WA KKAM KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI ASIMAMISHWA KAZI, SABABU NI HIZI....
Автор: WATETEZI TV
Загружено: 2025-09-19
Просмотров: 1180
Описание:
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) amemsimamisha kazi Askofu wa Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini, Dk. Edward Mwaikali, kuanzia Septemba 17, 2025, hadi pale Halmashauri Kuu ya Kanisa hilo itakapokaa na kujadili suala hilo.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia barua ya Katibu Mkuu wa KKAM yenye kumbukumbu namba KKAM/MSH0109/25 ya tarehe 17/09/2025, ikieleza kuwa Askofu Mwaikali hataruhusiwa kutoa huduma yoyote ya kiaskofu ndani ya kanisa hilo. Sababu zilizotolewa ni pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu kwa kufuata sheria na kanuni za kikatiba za KKAM, jambo lililosababisha uvunjifu wa amani ndani ya kanisa na kukiuka pia sheria za nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Askofu Msaidizi wa Dayosisi ya Nyanda za Juu Kusini, Nyibuko Mwambola, amethibitisha kupokea barua hiyo kutoka kwa Katibu Mkuu, na kuongeza kuwa Kamati Kuu tayari imekutana kujadili maelekezo yaliyomo.
Hata hivyo, katika hatua nyingine, baadhi ya wachungaji na waumini wa Parishi ya Ruanda wamezungumzia maamuzi hayo. Wakati huo huo, Askofu Dk. Mwaikali ameeleza kuwa hajapokea rasmi barua yoyote kutoka kwa uongozi wa juu wa kanisa, akisisitiza kuwa yeye ndiye aliyehusika katika kuanzisha KKAM.
Ikumbukwe kuwa Dk. Mwaikali pamoja na msaidizi wake, Askofu Nyibuko Mwambola, walisimama na waumini kadhaa kujitoa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kuanzisha KKAM. Hatua hiyo ilitokana na mgogoro wa ndani kuhusu uhamisho wa makao makuu ya Dayosisi kutoka mjini Tukuyu kwenda Usharika wa Ruanda, Jimbo la Magharibi
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: