ZMA YAJIPANGA KUKIDHIBITI KISIWA CHA CHUMBE
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-05
Просмотров: 1732
Описание:
Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) imesema inakusudia kudhibiti uharibifu wa mazingira unaoendelea kujitokeza katika maeneo ya bahari yanayozunguka Kisiwa cha Chumbe, kwa lengo la kulinda usalama wa kisiwa hicho pamoja na rasilimali zake za asili.
Akizungumza katika kikao cha awali kilichowakutanisha wadau mbalimbali kujadili changamoto za kimazingira zinazoikabili bahari ya Chumbe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Bandari na Meli kutoka ZMA, Salma Suleiman, amesema uharibifu mkubwa umetokana na baadhi ya vyombo vya usafiri wa baharini kuingia katika maeneo ya hifadhi kinyume na taratibu zilizowekwa.
Ameeleza kuwa hatua madhubuti zinahitajika kuchukuliwa ili kudhibiti vitendo hivyo vinavyohatarisha mifumo ikolojia ya bahari na uhai wa rasilimali zilizopo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mafunzo na Teknolojia kutoka Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), Kepteni Hussein Ali Makame, amesema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa athari kubwa za uharibifu wa mazingira katika bahari ya Chumbe, hali inayohitaji ushirikiano wa karibu kati ya taasisi husika na wadau wa mazingira.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: