KIWANDA CHA KUTENGENEZA KARATASI NA PLASTIKI CHAZINDULIWA MKURANGA
Автор: Main Digital
Загружено: 2025-05-27
Просмотров: 333
Описание:
#HABARI Serikali kupitia Kituo cha uwekezaji Tanzania-TIC imeendelea kuweka mazingira wezeshi yanayochagiza uwekezaji nchini hali inayovutia wawekezaji kuanzisha viwanda katika maeneo mbalimbali na hivyo kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kiwanda kipya cha kutengeneza karatasi, bidhaa za plastiki na za majumbani kinachimilikiwa na kampuni ya Goodwill AbdulWahid Mohammed ambaye ni mwanzilishi wa eneo la viwanda la kusini mwa Tanzania amesema kuwa kiwanda hiko kitakuza kilimo cha Mihogo katika maeneo hayo kwa kuwa ndiyo malighafi kubwa inayohitajika katika uzalishaji wa karatasi
Kwa upande wake meneja uhusiano kwa umma kutoka kampuni ya Goodwill Sharifa Chen amesema kiwanda hiko kilichopo kijiji cha mkiu wilaya ya mkuranga kitazalisha aina mbalimbali za karatasi huku akieleza kuwa mkakati ni kuwajengea uwezo watanzania kufanya kazi za kitaalamu na hivyo kupunguza ajira za wageni kiwandani hapo
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Mkiu amewataka wakazi wa maeneo hayo hususan vijana kujitokeza kuchangamkia fursa za ajira kiwandani hapo huku mmoja wa wananchi akishukuru uwepo wa kiwanda hiko kwani kitasaidia kuboresha maisha yao
#mainfmcup2025
#mainfmupdates
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: