Bembea Ya Maisha || Sehemu Ya Pili || Onyesho La Kwanza || Neema na Sarah
Автор: HOME of REALERS
Загружено: 2023-11-10
Просмотров: 15498
Описание:
Kitabu hiki kinazungumzia jinsi maisha yanavyoendelea kusonga mbele na kurudi nyuma kama bembea.
Kwa wale wasiofahamu, tafsiri ya neno bembea kwa kingereza ni 'swing'
Unakumbuka, kile kichezeo ulichozoea kukalia ulipokuwa mdogo na kuomba familia yako au rafiki akusukume ili uweze kuruka juu?
Ulipokuwa juu ulihisi kama unaweza kugusa anga.
Ulipokuwa nyuma ulilazimika kusukumwa mbele.
Hiyo ni angalau hadi ujifunze kujisukuma mbele kwa miguu yako unapokua.
Ahh, sasa umeifahamu?
Kama bado jua kuwa 'bembea' ni kifaa kama vile ubao, kamba au chuma inayoning'inia baina ya chuma au mti ambacho hutumiwa kuchezea aghalabu na watoto.
Kupitia wahusika mbalimbali kama Sara, Yona, Bunju, Neema na wengineo, mwandishi anatuonyesha na kutueleza jinsi wakati mwingine maisha yanavyoweza kujaa furaha na mara nyingine kujaa matatizo yanayosababisha maumivu na huzuni.
Kimsingi, maisha yana panda shuka zake. Wakati mwingine tuko juu na tunahisi kama tunaweza kugusa anga na wakati mwingine tuko chini.
Direct translation Basically, life has ups and downs. Sometimes we are up and we feel like we can touch the sky and other times we are down
Mwandishi kwa kutumia sitiari ya bembea pia anatuambia jinsi wakati mwingine kama tu wakati wa kubembea tunahitaji msaada.
Msaada kwa namna ya mtu wa kutusukuma mbele ili bembea letu lisikae palepale.
Baada ya yote, maisha hubadilika
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: