A - Z Sakata la Ras Inno Mikononi mwa Polisi
Автор: The Chanzo
Загружено: 2022-09-28
Просмотров: 814
Описание:
Ras Inno ni msanii mkongwe wa muziki wa miondoko ya Reggae, mtetezi wa haki za wabunifu ambaye pia ni Katibu wa Taasisi ya Mtandao wa Sekta Bunifu, au kwa kimombo Creative Industry Network Tanzania, (CINT).
Mnamo asubuhi ya Agosti 30, 2022, iliripotiwa kwamba polisi mkoani Iringa walimkamata Ras Inno akiwa nyumbani kwake na kumpeleka katika kituo kikuu cha polisi Iringa na kisha kuachiwa mchana wa tarehe hiyo hiyo bila kufunguliwa mashtaka. Kukamatwa kwake kunatokana na kufananishwa na mtuhumiwa mwingine.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CINT, Ras Inno hakuruhusiwa kuiaga familia yake, alishambuliwa na kudhalilishwa akiwa katika gari la polisi lililompeleka kituoni na pia akiwa kituoni. CINT ilidai pia kwamba Ras Inno aliumia kidogo sehemu ya mdomoni.
CINT pia iliripoti kwamba alipofikishwa polisi Ras Inno alishinikizwa kuimba baadhi ya nyimbo zake kama sehemu ya utambulisho wake. Pia, askari kituoni hapo wamelalamikiwa kumtishia kumyoa nywele zake aina ya rasta jambo ambalo CINT ilisema linadhalilisha imani yake.
The Chanzo ilifanya mahojiano maalum na Ras Inno kuweza kufahamu zaidi kuhusu haya na mengineyo mengi.
Unaweza kutufuatilia kupitia;
TWITTER: / thechanzo
INSTAGRAM: / thechanzo
FACEBOOK: / thechanzo
TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com
Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo Initiative, 2022 © All Rights Reserved.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: