SERIKALI INATAMBUA WATUMISHI WACHAPAKAZI - DKT. MWIGULU
Автор: KASACO MEDIA (K.T.S)
Загружено: 2026-03-10
Просмотров: 31
Описание:
SERIKALI INATAMBUA UWEPO WA WATUMISHI WACHAPAKAZI - DKT. MWIGULU
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inatambua uwepo wa watumishi wa umma wanaochapakazi na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu huku wakijiepusha kujiingiza katika makundi ya wazembe, wezi na wanaofanya kazi kwa mazoea.
“Serikali haitomuonea mtu, watumishi wachapakazi wasiingie ubaridi kwa sababu Serikali inatambua mchango wao katika maendeleo ya Taifa. Watu wasome alama za nyakati Serikali haitovumilia masuala ya wizi kwa sababu yanarudisha nyuma maendeleo.”
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Machi 09, 2026 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Namanyere wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Rukwa. Miongoni mwa malengo ya ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kuwasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi na kujiepusha na vitendo vya udokozi kwa sababu havikubaliki na havivumiliki, hivyo wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ikiwemo kusimamia ipasavyo ujenzi wa miradi.
Pia, Waziri Mkuu amesisitiza mikoa yote kuhakikisha katika upangaji wa bajeti wanaweka vipaumbele vya uchimbaji wa visima kupitia mitambo iliyosambazwa katika mikoa yao. “Mitambo ya uchimbaji maji itumike kuchimba visima ili wananchi wapate maji ya uhakika.”
Kadhalika, Mheshimiwa Waziri Mkuu amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa kufanya uchunguzi wa haraka kuhusu manunuzi ya vifaa vilivyotumika katika ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Amali ya Mkoa wa Rukwa, baada ya kubainika baadhi ya majengo kuwa na nyufa na kuwepo kwa tuhuma za baadhi ya vifaa kununuliwa kwa bei kubwa kuliko ya soko.
“Kamanda wa TAKUKURU wa Mkoa nenda kachunguze haya majengo ninayosema, kachunguze vifaa vimetokea wapi vimenunuliwa wapi na bei yake ikoje kulinganisha na sokoni. Mambo ya uholela hayakubaliki."
SUBSCRIBE NOW NA BONYEZA ALAMA YA KENGELE🔔 UWE WA KWANZA KUONA👉
/ @kasacomedia
============================================================
⚫️ JE, NA WEWE UNA SWALI AU JAMBO LOLOTE?
⚫️ WASILIANA NA KASAKO MEDIA : ( +255 761984534 )| Kimataifa: +1 317-519-5285
⚫️ Email: [email protected] | [email protected]
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo na Burudani Tanzania!
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW
⚫️ Kwa UPDATES zaidi,Subcribe kasako media
⚫️ Youtube / @kasacomedia
Project on the lives of artist and more|
@Kashindi Msambilwa| CEO/FOUNDER
@Sangani Fikiri. | CEO/FOUNDER
@Jerome Bucuma Paul | General Manager
@Richard Wakona | General Manager
@Emmy Joel Mwaipopo | Program Manager
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: