KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 09/ 10/ 2024
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2024-10-09
Просмотров: 3184
Описание:
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA EVENING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 09/ 10/ 2024
UJUMBE WA LEO: NAMNA UFALME WA MUNGU UNAVYOTUWEZESHA KUSHINDANA ILI KUSHINDA
Yeremia 1 : 19
Kutoka 17 : 8 - 16
1 Samwel 30 : 1 - 8
Kumbu kumbu 25 : 17 - 19
Yeremia 1 : 19
19 Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe.
Kutoka 17 : 8 - 16
8 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.
9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.
10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.
11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.
12 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.
14 Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.
15 Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;d
16 akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.
1 Samwel 30 : 1 - 8
1 Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;
2 nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao.
3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka.
4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena.
5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli.
6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.
7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko.
8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.
Kumbu kumbu 25 : 17 - 19
17 Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;
18 jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.
19 Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.
AMALEKI NI ADUI WA WA HATIMA YA ISRAEL AMALEKI NI ADUI WA NJIANI
NI ROHO ISIYOSHULIKA NA WATU WALIOKO UTUMWANI BALI INASHULIKA NA WATU WANAOTOKA UTUMWANI.
NI ROHO ISIYOPENDA UONE NYUMBANI NI MAHALI PA KUKALIKA AU NI ROHO INAYOPAGEUZA NYUMBANI MAHALI PA HUZUNI
1 Samwel 30 : 1 - 2
1 Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;
2 nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao.
Kumbukumbu 25 : 18 - 19
18 jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.
AGENDA ZA MAOMBI.
(1) OMBA AU MUOMBE MUNGU AMTIE NGUVU(JITIE NGUVU KATIKA BWANA)
(A) KATAA KUCHOKA
(B) KATAA KURUDI NYUMA AU KURUDISHWA NYUMA
(C) KATAA KUZIMIA
(2) OMBA KINYUME NA AMALEKI
(NENDA NA SHAMBULIA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO)ILI KUREJESHA MATEKA YALIO TEKWA NA ADUI AMALEKI.
(A) ONDOSHA ROHO YA MAFARAKANO
(B) MGAWANYIKO KUKOSA MKONO WA SHIRIKA
(C) MAUTI ILIYOKUSUDIWA KAMA MKAKATI WA AMALEKI
(D) KUKATISHWA TAMAA
Mhubiri: Mwl. Renald Mlawi
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe: [email protected]
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: